Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Baada ya mihula miwili ya uongozi, Bouteflika alibadilisha Katiba, ambayo ilimruhusu kusalia madarakani kwa muhula wa tatu, kisha muhula wa nne ambao aliuanza akitembea kwa kutumia kiti cha magurudumu, baaada ya kupata ugonjwa kiharusi mnamo 2013.
Baada ya kutangaza nia yake ya kuwania kwa muhula wa tano, maandamano ambayo hayajawahi kutokea yaliibuka nchini Algeria. Baada ya kuonekana kuwa ni dhaifu na afya yake inaendelea kuzorota, Abdelaziz Bouteflika alilazimishwa kujiuzulu na mkuu wa jeshi Aprili 2, 2019, baada ya wiki sita za maandamano makubwa ya wananchi. Siku hiyo alionekana kwa mara ya mwisho kwenye runinga akitangaza kwamba anaachia ngazi. Abdelaziz Bouteflika, alikuwa kiungo muhimu katika vita vya kupigania uhuru wa Algeria katika muongto wa 50 na 60.
Harakati zake za kisiasa zilianza mapema kwani baada ya uhuru wa Algeria kutoka kwa mkolini Ufaransa mwaka 1962, alikuwa waziri mdogo zaidi wa Mashauri ya Kigeni, rekodi ambayo haijavunjwa hadi wa leo.
Bouteflika aliishi uhamishoni katika miaka ya 80, kuepuka mashtaka ya ufisadi dhidi yake ambayo mwishiwe yalifutwa.
Alirejea nyumbani miaka ya 1990 na kuchukua hatamu ya uongozi mwaka 1999 - kama kiongozi wa kwanza wa kiraia wa Algeria.
342/